Tuesday, February 12, 2013

UMAKINI BARABARANI HASA KWA WAENDESHA BODABODA

Ukiwa kama dereva wa chombo cha moto, unaweza kuwa makini barabarani lakini akatokea dereva mwingine akakusababishia ajali bila kutarajia, kama ajali hii ilivyotokea.

Majira ya saa mbili asubuhi gari aina ya Suzuki namba T 845 AAL, wakati dereva wake ambaye ni mwanamama alipokuwa akijitahidi kumkwepa mwendesha pikipiki (bodaboda), yakamkuta mengine. 







Ajali hii imetokea katika barabara ya Nairobi mbele ya kituo cha mafuta cha Oilcom - Sakina, baada ya jitihada zote za Mwanamama aliyekuwa akiendesha gari hili kumkwepa mwendesha bodaboda kushindikana na hivyo kutumbukia katika mtaro huo wa maji. Dereva wa gari hili amepata majeraha kidogo mwilini ingawa mshtuko pia ulimpata.

Picha na Mpiniwashoka blog.

No comments:

Post a Comment