HABARI NJEMA KWA MFUGAJI
Katika pitapita zangu kwenye mabanda ya maonyesho ya kilimo nane nane katika viwanja vya TASO Njiro - Arusha, nikakutana na kitu kilichonivutia katika banda la Halmashauri ya wilaya ya Arusha - Arusha DC, nikaona ni vema kama nitaweza kukushirikisha ewe mfugaji wa mifugo ya nyumbani mfano kware, kuku, mbuzi na hata ng'ombe, kutumia teknolojia mpya inayoitwa HYDROPONICS.
HYDROPONICS ni teknolojia ya kuotesha mazao kwa maji na virutubisho bila kutumia udongo.
FAIDA ZAKE: Ni rahisi kutumia teknolojia hii kwani inaweza kufanyika mahali popote. Husaidia kuvuna na kupata mazao mengi kwa muda mfupi. Haina madhara kwa afya za mifugo na binadamu kma mlimaji alizingatia maelekezo.
Hutumia kiwango kidogo cha maji na haihitaji udongo, huku ikiokoa matumizi ya ardhi.
HYDROPONICS FODDER - ni kimea kinachooteshwa kwa kutumia mbegu za shayiri ili kupata chakula cha mifugo mfano kuku, ng'ombe, sungura, nguruwe, mbuzi, kondoo n.k.
Ili kuotesha mbegu zako kwa utaratibu huu utahitaji kuwa na banda maalum kwa kuoteshea lenye ukubwa wowote, trei za plastic au aluminium zenye matundu (kama ni aluminium hakikisha sio material yale yanayopata kutu pindi yakiingia maji).
Pia utahitaji kuwa na virutubisho vya hydroponics (Hydroponics Nutrients), Sprayer (Chupa ya kunyunyiza maji yenye matundu madogo ili maji yamwagike kama mvua), Mbegu za Shayiri au ngano (chagua mbegu ambazo hazijashambuliwa na wadudu), na pia unatakiwa uwe na chombo cha kuloweka mbegu na hapa waweza kutumia ndoo ya aina yoyote, kwani itatakiwa uziloweke kwa siku chache.
Kwa maelezo ya kitaalamu zaidi wasiliana na namba hii 0766 503 330
No comments:
Post a Comment