Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict XVI, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ifikapo tarehe 28 mwezi wa pili mwaka huu.
Habari kutoka Vatican zinasema kuwa, sababu ya kiongozi huyo kujiuzulu ni kutokana na afya yake kuendelea kudhoofika.
Papa Benedict XVI mwenye umri wa miaka 85, alichaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki tarehe 19/04/2005 baada ya kifo cha Papa John Paul wa pili, na anakuwa kiongozi wa pili wa Kanisa hilo kujiuzulu baada ya Celestine V kujiuzulu mwaka 1292 kutokana na sababu za kiafya.
Ingawa Vatican imesea sababu za kutaka kujiuzulu kiongozi huyo ni umri wake mkubwa, lakini wadadisi wa mambo wanaamini kuwa kashfa mbalimbali zilizotokea katika Kanisa Katoliki chini ya uongozi wake ni miongoni mwa sababu ya yeye kuchukua uamuzi huo.
Chanzo: iran swahili radio
No comments:
Post a Comment