Kwa mujibu wa Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka UNESCO - Tz, bi Rose Haji Mwalimu, lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi wa mawakala wa redio za jamii (Correspondents) katika kukusanya habari na taarifa mbalimbali kwa lengo la kupanua wigo wa upashanaji wa habari kijiografia na kukuza uelewa wa wananchi kwa masuala mbalimbali ya maendeleo yao na taifa kwa kutumia teknolojia mpya (TEHAMA).
Mbali na hilo, Bi Rose ameyataja malengo mengine kuwa ni kutathimini umuhimu wa kupanua wigo wa upashanaji wa habari, kutambua njia mbalimbali zinazotumika katika ukusanyaji wa habari na taarifa, na kuelewa umuhimu wa kuandika habari za ukweli, uhakika na bila kupendelea upande wowote.
Malengo mengine ne kupambanua mbinu mbalimbali za kuendesha mahojiano, kutathimini aina gani za habari zinalinda heshima na zisizolinda (Good and Bad Taste) kuwa na uwezo wa kuchangia katika vituo vya redio, kuanzisha mtandao wa wachangiaji katika kutafuta habari za redio jamii na kuonyesha uwezo wa kukusanya habari na taarifa mbalimbali kwa vitendo.
Mafunzo hayo ya siku 5 yamezishirikisha redio za jamii za Fadeco - Karagwe, Kahama fm - Kahama, Sengerema Redio - Sengerema, na Redio jamii Orkonerei - Simanjiro kwa kundi la kwanza ambapo mafunzo mengine yalifanyika Kyela na kuzihusisha redio jamii za Kyela fm - Kyela, Pambazuko fm - Ifakara, Pangani fm - Pangani Tanga, Mtegani redio - Makunduchi Unguja na Redio Jamii Micheweni - Pemba.
Mafunzo haya yataendelea kufanywa kwenye redio za jamii tofauti tajwa hapo juu ambazo zipo 9 na zipo kwenye mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na SIDA wa kuwezesha redio za jamii ziliingia kwenye mradi huo wa miaka mitatu kwa kupatiwa mafunzo mbalimbali.
HABARI PICHA
Mwezeshaji wa mafunzo Bi Rose Haji Mwalimu, kutoka UNESCO katika vazi la Kimasai
Mwezeshaji mafunzo msaidizi Khadija Abdallah kutoka ORS fm - Terrat
Picha chini ni washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Mtaani wakifanya kwa vitendo yale waliyofundishwa (wakiwa katika makundi)
Baada ya kazi ya kurekodi sasa ni wakati wa kutengeneza kazi hiyo ili ipatikane kipindi
Hii ni picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo.
No comments:
Post a Comment