Wadau watano wa ORS fm - Simanjiro tuliungana wadau wanne kutoka Kahama Fm kuelekea Karagwe - Kagera.
Tulipiga kambi kwa muda eneo linaloitwa BENAKO kwa ajili ya kupata chochote kabla ya kuendelea na safari
William Bundala (Kijukuu cha bibi K) na Ramadhan Zuberi (Dj Rammy) kutoka Kahama fm, tuliungana nao kwa safari hiyo ya Karagwe.
Julius Laizer, Agnes Utou na Kijukuu wakipata supu eneo la Benako
Joyce Elias na Kijukuu wakiwaza kufika Karagwe, baada ya kuambiwa hakuna kuna shida ya usafiri kwa siku ya Jumapili kutoka Benako to Karagwe.
Wadau wakiwa bize, kubadilishana mawazo
Tulikuwana naye Benako, alitustorisha hadi raha
Kijukuu akiangalia uchomaji wa ndizi na maganda yake - Tembea ujionee na kujifunza zaidi.
Safarini, mwendo wa zaidi ya saa 4 kufika Karagwe
Geti la kwanza
Unaweza usiamini, lakini ndivyo hali ilivyo kwa walinda usalama wa hii njia
Mambo yetu yaleee ya dawa za kiasili
Hapa ni kwenye geti la pili, nyumba kama hizo zipo saaaana hata mitaa fulani hivi kwa wale wenzetu
Aaaah wewe usinipige picha bwana, ndivyo alivyokuwa akisema bwana Sadiq, safari tuliiona fupi sababu ya huyu jamaa, anaongea hakaukiwi maneno, much respect kwako bwana Sadiq kwa kampani yako.
Ulishawahi sikia pori ambalo Kamanda Tossi alikuwa anapambana na majangili, watekaji magari waliokuwa wanawaimbisha abiria Mtaji wa Maskini ni nguvu zake mwenyewe, ndio njia hiyo, asikwambie mtu hili pori hadi ulimalize na kufika salama Karagwe ni jambo la kumshukuru mungu, hapa tulisindikizwa na escort ya askari kwa kila geti wakipokezana hadi mwisho wa safari.
Hatimaye tukaanza kuona unafuu wa kufika
Kutoka kushoto ni Jackson Massawe (ORS fm) Sebastian Furaha a.k.a Seba, Khadija Hassan - culture lady (Kahama fm) Julius Laizer, Khadija Abdallah, Agnes Utou (ORS fm) mwenye kofia ni Ramadhan Zuberi a.k.a Dj Rammy na aliyechuchumaa ni William Bundala - Kijukuu cha Bibi K (Kahama fm) tukipozi.
Zao maarufu (Ndizi Bukoba, Matoke n.k) hapa ni njia ni tukielekea Kayanga.
Panapendeza
Tanzania yetu ni nzuri mnooooooo
Aina ya upandaji Kahawa na Migomba
Mambo ya msosi hayooooo. Ndizi zilizosongwa zimechanganywa na njegere, ndo msosi tulikaribishwa nao.
Nafurahia
ReplyDelete