Tuesday, February 12, 2013

UGUMU WA MAISHA WACHOCHEA KASI YA UKATAJI MITI KWA AJILI YA UCHOMAJI MKAA

Pamoja na Serikali kujipanga kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini, biashara ya uchomaji mkaa bado inashamiri kila kukicha hapa nchini. Uharibifu wa mazingira umekuwa mkubwa sana na madhara yake yamekuwa wazi sana kwenye baadhi ya mikoa, misitu imetoweka kutokana na ukataji miti hivyo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Baadhi ya wachoma mkaa katika kijiji cha Mwendakulima  - Kahama. 





Ni maarufu kwa jina la Mwanavere, ni mwanamke maarufu mchoma mkaa ambaye alinieleza kuwa sababu za kifamilia ndiyo chanzo kikubwa cha kujishughulisha na biashara hiyo, anaenda porini, anakata miti, magogo na kuyaweka kwenye tanuri mwenyewe.


Hii ni nyumba ya Mwanavere katika kijiji cha Gongwa - Kahama, ambayo ameijenga kutokana na biashara hiyo ya uchomaji wa mkaa, anaishi na watoto wake.


Mwanavere akiwa na baadhi ya watoto wake, ana watoto saba wote wa kike, akiwa amepozi nao mbele ya nyumba yake. Mwenye Tshirt nyekundu ni mtangazaji wa Redio Kahama William Bundala ambaye alinipeleka kumuona Mwanavere (Shukran sana).


NB:
Panda miti kata mti.

No comments:

Post a Comment