Thursday, August 09, 2012

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MANYARA NA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO KATIKA KIJIJI CHA TERRAT KUHAMASISHA KUHUSIANA NA SENSA YA WATU NA MAKAZI


Picha ya juu Msafara wa mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo ukiwasili katika kijiji cha Terrat.

Afisa matangazo ya nje (PA system) wa redio ORS fm na kampuni ya Orkonerei Mass Media (ORMAME) Greyson Martin akiweka sawa vifaa kwa ajili ya kuwezesha usikivu mzuri wa mahojiano wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Simanjiro na mkuu wa mkoa wa Manyara.


Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo akifungua mkutano na kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Simanjiro.


Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo akisalimia wananchi na kisha kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Manyara (aliyeinama).


Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo akisalimia wananchi na kisha kutoa nasaha kwa ajili ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 26/08/2012 kote nchini.







Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo na mkuu wa wilaya ya Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo kuhusiana na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi katika kijiji cha Terrat.





Baadhi ya wananchi wakiuliza maswali kuhusiana na taarifa za sensa ya watu na makazi na namna mifugo yao itakavyohesabiwa ilhali wangine wako mbali na hata nje ya wilaya ya Simanjiro.


Diwani wa kata ya Terrat Robert Saitabau akiongea na wananchi wakati wa uhamasishaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo (kushoto), mwenyekiti wa kijiji cha Terrat Supuk Nelukendo (katikati) na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro Brown Ole Suya (kulia) wakifuatilia jambo wakati wa mkutano na wananchi kuhusiana na uhamasishaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 26/08/2012 hapa nchini.

Afisa utamaduni wilaya ya Simanjiro bwana Lameck Nanyaro akimsomea taarifa ya mkuu wa mkoa wa Manyara na mkuu wa wilaya ya Simanjiro (hawapo pichani) juu ya washiriki wa mafunzo ya waratibu wa sensa ya watu na makazi katika shule ya sekondari ya kata ya Terrat. Nyuma waliosimama ni washiriki wa mafunzo ya uratibu wa sensa ya watu na makazi.

****
Zoezi la sensa ya watu na makazi linatarajiwa kufanyika hapa nchini tarehe 26/08/2012 baada ya miaka kumi ambapo lilifanyika mara ya mwisho mwaka 2002. 

Katika ziara yake ya kutembelea wilaya ya Simanjiro na Mkoa wa Manyara, mkuu wa mkoa wa Manyara Elasto Mbwilo amewataka wananchi hao kujitokeza kuhesabiwa siku hiyo ikifika na kuachana na dhana iliyojengeka kwa wengi kuwa kuhesabiwa kunasababisha kifo kwa mifugo na watu.

Pia ameitaka jamii ya kifugaji kuachana na kilimo cha zao moja la mahindi pekee bali wachanganye mazao mbalimbali katika mashamba hasa yale yanayostahmili ukame, ili waweze pia kujihifadhia mazao yao kwa chakula cha baadaye na kuondokana na kubweteka huku wakisubiria chakula cha msaada.

Amewahakikishia wananchi wa Simanjiro kuwa endapo watapanda zao la mtama na wakakosa mahali pa kuuzia yeye yupo tayari kuwatafutia soko la zao hilo au pia atawabadilishia na mahindi ili kujiepusha na chakula cha msaada.

Mkuu huyo wa mkoa wa Manyara anaendelea na ziara yake katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Simanjiro.


NB:

Picha na Greyson Martin na Baraka David Ole Maika

No comments:

Post a Comment