Thursday, November 27, 2014

HOUSE GIRL ALIYEMTESA MTOTO UGANDA KUFIKISHWA MAHAKAMANI DISEMBA 8, 2014

Mfanyakazi wa nyumbani Jolly Tumuhirwe wa Uganda aliyekamatwa kwa kosa la kumfanyika mtoto ukatili, anatarajiwa kufikishwa mahakani tarehe 8 Disemba.

Jolly ambaye anashikiliwa katika gereza la Luzira nchini Uganda, alikamatwa baada ya kukimbilia polisi kumshtaki mwajiri wake ambaye alimpiga kufuatia kitendo cha kuona video inayoonyesha namna mwanae alivyokuwa akitendewa na msichana huyo. 

Polisi walimkamata bwana Erick Kamanzi ambaye ni baba wa mtoto na baada ya kufikishwa kituo cha polisi alieleza sababu za kumpiga msichana huyo na kuwaonyesha video.




Tumuhirwe baada ya kuona video hiyo iliyonaswa na  kamera ya CCTV , alikubali kosa na polisi walipomfanyia uchuguzi wa kiakili walibaini kuwa ana akili timamu.

Afisa mkuu wa polisi Uganda Fred Enaga, amewaomba waajiri kuchunguza mbinu zitakazotumika kuwachagua wasichana wa kazi kwani matendo kama haya yanaweza kutokea kutokana na matatizo ya kisaikolojia.


Baba wa mtoto bwana Erick Kamazi akiwa na watoto wake, Kulia ni mtoto aliyeteswa na msichana wa kazi.

No comments:

Post a Comment