MKUFUNZI WA SEMINA MWALIMU ROSE HAJI AKITOA DARASA KWA WAANDISHI WA HABARI MJINI KAHAMA.
KAHAMA
Uhusianao mbaya miongoni mwa waandishi wa habari ndiyo
chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili ya taaluma ya hiyo nchini.
Hayo yamebainishwa leo na Mwandishi mkongwe nchini ambaye
pia ni mkufunzi wa semina ya siku tano ya waandishi wa habari inayoendelea
mjini kahama mama rose Haji Mwalimu kupitia shirika la UNESCO.
Haji amesema kuwa waandishi wa habari wengi nchini
wamekuwa na chuki miongoni mwao hali inayopelekea kuchafuana na kujengeana
uhasama katika vyanzo vya habari.
Ameongeza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuweka
ushindani katika kutafuta habari na kulikomboa taifa katika matatizo mbalimbali
na si kijijengeana chuki hali, itakayopelekea kukosa uamnifu na kudhalaulika
katika jamii.
Kwa upande wao waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo
hayo wamekiri kuwepo kwa tabia hiyo kwa baadhi ya waandishi na kudai kuwa, sababu kubwa inayopelekea hayo
ni baadhi ya watu kuingia katika fani ya uandishi pasipokuwa na taaluma.
Mafunzo hayo ya siku tano yanayojumuisha washiriki ishirini
kutoka Redio za KAHAMA, FADECO ya KAREGWE,SENGEREMA ya MWANZA na ORKONEREI ya SIMANJIRO ni
mwendelezo wa mafunzo ya uhariri na mipango ya vipindi chini ya mradi wa miaka
mitatu unaoendeshwa na shirika la
UNESCO.
WAANDISHI WAKIENDELEA NA MAFUNZO
WAANDISHI KUTOKA VITUO VYA FADECO RADIO NA SENGEREMA WAKIENDELEA NA MAFUNZO.
WAANDISHI WA HABARI KUTOKA RADIO MBALIMBALI WAKIWA KWENYE CHUMBA CHA SEMINA.
KUTOKA KUSHOTO NI SEBASTIANE FURAHA WA RADIO KAHAMA,KATIKATI NI
FEBRONIA BILIKWIJA WA RADIO SENGEREMA NA ENDRUE MFUNGO WA SENGEREMA FM.
KUTOKA KUSHOTO NI JOYCE ELIUS WA ORS FM,KIJUKUU CHA BIBI K WA RADIO KAHAMA FM,RACHEL LEMBURIS WA ORS FM NA AGNES UTOU
TOKA KUSHOTO KHADIJA KHASSAN WA KAHAMA FM,SEBASTIANE FURAHA KHM FM NAFEBRONIA WA SENGEREMA FM.
MKUFUNZI WA SEMINA MWL ROSE HAJI AKICHUKUA KUMBUKUMBU YA PICHA KABLA YA SEMINA KUANZA.
WASHIRIKI KUTOKA RADIO FADECO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.
No comments:
Post a Comment