Wednesday, August 29, 2012

SHEREHE YA TOHARA




Baadhi ya vijana wa kabila la kimaasai maarufu kama Skolio wakiwa wamepozi wakati wa sherehe ya wenzao waliokuwa wameingia jandoni (hawapo pichani).

Vijana wa kabila la kimaasai (Skolio) katika kijiji cha Loiborsoit-Simanjiro, wakiwa wamejichora na kuvaa manyoya ya ndege kichwani na mgongoni, kwa imani kuwa kwa kufanya hivyo wanajizuia na watu wenye macho mabaya (maarufu kama Zongo).

MAAKULI NAYO HAYAKUKOSEKANA KATIKA KUSINDIKIZA SHEREHE HIYO


Baadhi ya kinamama wakirekebisha masuala ya msosi katika sherehe hiyo ya tohara kwa vijana wa kabila la kimaasai katika kijiji cha Loiborsoit A.

NYAMA NAZO HAZIKUKOSEKANA KAMA ILIVYO JADI YA KABILA LA KIMAASAI





Baadhi ya wazee wa kimaasai wakikatiwa nyama kama ilivyokawaida kushirikiana japo kila mmoja apate mnofu.

Mzee wa boma ilipofanyika sherehe ya tohara katika kijiji cha Loiborsoit A, Ndugu Yohana Shinini akikaribisha wageni waliohudhuria.


SURA YA KAZI

Afisa matangazo ya nje PA wa ORS fm Greyson Orongai akiwa amepozi kufuatilia kila kinachoendelea katika sherehe hiyo.


ALIYEGUSWA
Akidhihirisha kuwa si kushika chaki tu pekee, huyu ni Mwalimu Elisha akionesha umahiri wa kucheza kiduku.

2 comments: