Sunday, November 18, 2012

TASWIRA KATIKA PICHA - VIONGOZI WETU WA KESHO




Hii ni taswira yetu ya leo katika picha, wakati watoto wengine huamka asubuhi na kukutana na maji ya moto ndani ya nyumba na mabomba yakitoa maji kwa wingi, sare nzuri za shule na  mtoto huyu wa kichungi tulimkuta katika eneo la Engaresero asubuhi akinawa tayari kwa kuelekea shuleni.


Hawa nao hivyo hivyo, walipoona gari linakuja maana gari lilivuka hapo (hakuna daraja) kwa kuingia ndani ya maji, ilibidi wapozi kwanza.

Hawa ni baadhi ambao walishamaliza zoezi la kunawa kama si kuoga kabisa, wakivaa nguo zao kwa ajili ya kuelekea shuleni.

Kweli hili ndilo taifa tunalolitegemea la baadaye, wanasoma katika mazingira magumu hasa jamii hii ya kichungi ambayo wengi wao wapo pembezoni.

No comments:

Post a Comment