Thursday, November 01, 2012

UZINDUZI WA JIJI LA ARUSHA

Tarehe 1 November 2012, ilikuwa ni siku muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Arusha, baada ya Rais wa Jakaya Kikwete wa Tanzania kulizindua rasmi jiji la Arusha pamoja na barabara zake.


Kushoto ni bendera  ya Jiji la Arusha na kulia ni bendera ya Tanzania.


Wakati wananchi wa Arusha wakisubiri ujio wa mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete, ghafla mvua kubwa ikaanguka na kusambaza wananchi waliokuwa katika mnara mwa Mwenge wakisubiria uzinduzi huo.


Mbwa wa polisi akipitishwa kufanya ukaguzi.

Wanafunzi wakitumbuiza kumkaribisha mgeni rasmi

Brass band wakiimba wimbo wa Taifa.

Huu ni uzinduzi wa Jiji la Arusha, lakini nilijiuliza kama kulikuwa na ulazima baadhi ya wananchi kuvaa mavazi yanayolenga vyama kama hawa.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi wa Jiji la Arusha kutoka kushoto waliokaa ni Waziri wa Ujensi Mh. John Maghufuli, Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Magesa Mulongo, Rais Jakaya Kikwete na Mh Hawa Ghasia (Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI).


NB: Hongera wana Arusha kwa kuzinduliwa na kuwa JIJI, La muhimu si kufurahia kuitwa jiji, ni wakati muafaka wa kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha Jiji linakuwa SAFI.

Shukran Julius Laizer kwa mapicha.

No comments:

Post a Comment