Friday, November 16, 2012

UTALII WA NDANI


Pichani ni mlima Oldonyolengai (mlima wa Mungu kwa kimaasai) ambao ni mlima pekee hapa nchini wenye Volcano ambao ni kivutio cha watalii hapa nchini.



Mlima huu haupandiki kirahisi na huchukua takribani masaa 5 au 6 kwa sababu ya vumbi na miamba inayoteleza katika mlima huu.


Kwa kawaida kama mtu anataka kuupanda huu mlima anatakiwa aanze safari yake saa tano au sita usiku ili aweze kufika alfajiri ungali bado umepoa.


Pichani juu ni vilima vingine viwili (kimoja chenye alama nyeusi juu) ambavyo navyo kutokana na volcano kurushwa navyo pia vimeshaanza kuvimba kama ishara ya kurusha volcano. Vilima hivi vipo pembeni ya mlima Oldonyolengai.

No comments:

Post a Comment