Kiwanda cha maziwa cha Ilaramatak - Terrat Simanjiro - Manyara
Picha juu na chini ni bwana Deusdedit Kalenzi (anayevaa boot) kutoka tume ya ardhi ya mipango TAMISEMI.
Sheria nje ya kiwanda lazima uvae buti, koti jeupe na kofia laini kichwani ndipo uingie, juu ni baadhi ya waheshimiwa wakitii sheria kabla ya kukaribishwa ndani.
Sharti mikono iwe safi ndipo kwa kusafisha na dawa maalum ndani ya kiwanda ili kuzuia maambukizi yoyote ya bakteria kwenye bidhaa zitokanazo na maziwa. (Pichani ni bwana Leo Mavika kutoka ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI) akisafisha mikono kwa dawa maalum
Kushoto ni bi Nasinyari Marko - Meneja wa kiwanda cha Maziwa Terrat akiwaelezea wageni (hawapo pichani) namna wanavyoendesha kazi zao za kila siku, kulia ni bwana Samwel Nangiria mratibu wa mtandao wa mashirika ya kiraia - NGONET wilaya ya Ngorongoro.
Kikazi zaidi nikijaribu kunasa sauti ya maelezo ya Nasinyari
Hizi ni Cheese ambazo ni baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hiki cha maziwa.
Camera Operator wa ORMAME Gideon John akichukua picha za kumbukumbu kwa ajili ya mradi wa Video wa ORMAME.
Ziara hii ya viongozi hawa kutoka TAMISEMI mi muendelezo wa ziara ya mafunzo waliyoifanya nchini Kenya kuangalia hali ya uchumi wa wafugaji na maboresho katika maeneo ya kifugaji nchini.
No comments:
Post a Comment