Friday, September 28, 2012

MAMA SHUJAA WA CHAKULA KUTOKA KARAGWE

Nilipokuwa Karagwe nilipata bahati ya kukutana na Bi Emeliana Aligaesha ambaye ni mmoja wa washiriki wa shindano la Maisha Plus Mama Shujaa wa Chakula kutoka Karagwe. 

Kina mama washiriki ni 15 kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, mwenyewe aliniambia wakati nafanya naye mahojiano, baada ya kujaza fomu za ushiriki, alikuja fahamu kuwa wapo 15 kupitia mtandao wa Internet ingawa ye si mtumiaji sana ila ilibidi aombe msaada wa matumizi ya Internet.


 Tukifanya mahojiano na Bi Emeliana

 Akituelezea namna migomba inavyotakiwa kupandwa kwa nafasi kiasi gani.


 Kwenye pozi na mama Emeliana

 Kutoka Kushoto ni Bi Emeliana Aligaesha - mshiriki wa mama shujaa wa chakula Karagwe, Seba - Kahama fm, Khadija na Jackson - ORS fm.

No comments:

Post a Comment